Jumatatu 11 Mei 2026 - 08:00
Mapambano ya Kiongozi Shahidi yamefungua upeo mpya wa mwamko na matumaini kwa Umma wa Kiislamu na wanadamu

Hawza/ Hujjatul Islam wal-Muslimin Sayyid Sajid Ali Naqvi, katika hotuba yake alisema: Fikra na juhudi za kimapambano za Ayatullah al-Udhma Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu, zimefungua upeo mpya wa mwamko, uelewa na matumaini kwa Umma wa Kiislamu na wanadamu wote.

Kwa mujibu wa Kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, hafla ya kuadhimisha kumbukumbu ya shahada ya Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Shahidi Ayatullah al-Udhma Sayyid Ali Khamenei, ilifanyika katika ukumbi wa Waandishi wa Habari wa Rawalpindi nchini Pakistan.

Kikao hicho kilihudhuriwa na kundi la wanazuoni, shakhsia za kidini na kitamaduni kwa lengo la kiuenzi nafasi tukufu ya mashahidi na kufafanua fikra za shahid kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu.

Katika hafla hiyo, Hujjatul Islam wal-Muslimin Sayyid Sajid Ali Naqvi, Rais wa Baraza la Wanazuoni wa Kishia Pakistan, huku akisema kwamba; Ayatullah al-Udhma Khamenei alikuwa shakhsia kamili yenye vipengele mbalimbali vya kifkra, aliongeza kuwa; yeye aliyafikisha Mapinduzi ya Kiislamu katika kilele cha ustawi na maendeleo, na akaufikisha kwa walimwengu ujumbe ulio wazi wa madhehebu ya Ahlul-Bayt (as), hususan fikra ya Husseini.

Aliongeza kuwa: Fikra hii imejengwa juu ya msingi wa kwamba; wafuasi wa madhehebu haya hawainamishi vichwa vyao mbele ya nguvu yoyote batili, na wanaona utamaduni wa shahada kuwa ni sehemu ya utambulisho wao wa kiimani na kihistoria. Na ndiyo sababu Jamhuri ya Kiislamu ya Iran chini ya uongozi wa Ali Khamenei, kwa kusimama imara na kufanya muqawama dhidi ya mashinikizo na uadui, imeweza kuthibitisha ukweli huu kwamba katika njia ya haki hakuna nafasi ya maridhiano wala kurudi nyuma; bali ukweli ni kwamba mwanadamu anapaswa kusimama pamoja na haki na kujitoa mhanga kwa ajili yake.

Mwanazuoni huyo mashuhuri wa Kipakistan, alibainisha kwamba; kuchunguza kwa kina na kwa usahihi mwenendo na fikra za Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu ni miongoni mwa mahitaji muhimu ya zama hizi. Pia alisisitiza kwamba; fikra na juhudi zake za kimapambano zimefungua upeo mpya wa mwamko, uelewa na matumaini kwa Umma wa Kiislamu na wanadamu wote.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha